Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mkutano huu umeandaliwa na Global Deaf Muslim Foundation (GDMF) Taasisi ya Kimataifa ya Waislamu Wasiosikia, mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hii pia alikuwa miongoni mwa washiriki wakuu wa mkutano huu.
Waislamu wengi wasiosikia hukabiliana na changamoto ya kutopata mkalimani pale inapohitajika, mara nyingi hufanya kila wawezalo kuwashawishi waajiri wao, lakini bado matatizo hubakia, mojawapo ya changamoto walizonazo ni kwamba baadhi ya wasiosikia wanatoka katika familia za wahamiaji, na huenda kutokana na hali yao ya kutosikia wasiweze kujifunza lugha ya nchi ya asili, na hivyo kutegemea kabisa lugha ya ishara.
Katika misikiti mingi, matumizi ya lugha ya ishara pale inapohitajika hayazingatiwi, hata katika khutba za Ijumaa, kwa kuwa elimu ya Kiislamu na ya kidini kwa kawaida hupitishwa kupitia njia za jadi za mdomo na kusikika, mara nyingi watu hawa hukabiliwa na ugumu wa kuzielewa na huhitaji msaada.
Chanzo: Cairo Scene
Maoni yako